Deborah raia wa Angola tulimsajili Julai mwaka jana kutoka Mutondo Stars ya Zambia kwa mkataba wa miaka mitatu.
Deborah (25) ni mchezaji mwenye uwezo mkubwa wa kucheza nafasi mbalimbali uwanjani lakini baada ya makubaliano ya pande zote hatakuwa sehemu ya kikosi chetu.
Advertisement
Deborah ni mmoja ya wachezaji ambao walikuwa wanatarajiwa kufanya makubwa kikosini kutokana na uwezo wake mkubwa ingawa leo tunaagana rasmi.
Uongozi wa klabu unamtakia Kheri Debora katika maisha yake mapya ya soka nje ya Simba.