Che Malone alijiunga nasi Julai 2023 kutoka Cotton Sports ya Cameroon na tangu hapo amekuwa muhimili mkubwa katika idara yetu ya ulinzi.
Che Malone (26) raia wa Cameroon alikuwa amebakisha mkataba wa mmoja lakini baada ya makubaliano baina yetu pamoja na USM Algiers sasa ni rasmi amejiunga na miamba hiyo ya Algeria.
Advertisement
Klabu ya Simba imekuwa muumini mkubwa wa kuwapa wachezaji wake nafasi kila kunapo patikana fursa mpya ili kuwafanya kupata mafanikio zaidi ya kiuchumi.
Simba inamtakia kheri Che Malone katika maisha yake mapya ya soka katika timu ya USM Algiers.