Tulisaini mkataba wa mwaka mmoja na Lukula na baada ya msimu kumalizika na kutofikiwa na malengo tuliyojiwekea tumeamua kutoendelea nae.
Tulikuwa na malengo ya kutetea ubingwa wa Ligi ya Wanawake ya Serengeti Lite Women's Premier League (SLWPL) lakini hayakufikiwa.
Advertisement
Msimu wa 2022/23 haukuwa mzuri kwetu kuanzia timu ya Wanawake hadi ya Wanaume na mpango uliopo sasa ni kuhakikisha tunarejesha kila kitu tulichopoteza.
Uongozi unaendelea na mchakato wa kutafuta kocha mpya wa Simba Queens na utakapokamilika atatangazwa mapema ili kuanza mara moja maandalizi ya msimu mpya wa ligi 2023/24.