Baleke amerejea katika timu yake ya TP Mazembe ya Dr Congo.
Katika kipindi chote alichokuwa ndani ya kikosi chetu Baleke amekuwa mshambuliaji kinara na alijitoa kwa kila hali kuhakikisha anasaidia timu kupata ushindi.
Kwa upande wake Phiri yeye anakwenda katika klabu ya Power Dynamos ya Zambia ambayo atakuwa huko hadi mwisho wa msimu.
Advertisement
Kabla yakupatwa na majeraha yaliomuweka nje ya uwanja kwa kipindi kirefu Phiri alikuwa chaguo la kwanza ndani ya kikosi.
Uongozi unaamini Phiri atakaporejea kikosini atakuwa imara zaidi na kurudi katika makali yake yaliotufanya kumsajili kutoka Zanaco FC ya Zambia.
Simba ina thamini mchango wa nyota hao na tunawakia kheri na mafanikio mema katika maisha yao mapya.