Ally alijiunga nasi akiwa kijana mdogo katika msimu wa 2016/2017 akitokea timu ya Makorora FC ya Tanga ambapo alijiunga na timu ya vijana.
Msimu wa 2017/2018 alipandishwa kwenye timu ya wakubwa ambapo amedumu mpaka tulipofikia makubaliano yapande mbili.
Advertisement
Ally amefanya kazi na makipa wakubwa mbalimbali waliopita ndani ya kikosi chetu kitu ambacho kimemjenga na kumfanya kuzidi kuwa bora zaidi.
Simba inamtakia kheri Ally katika maisha yake mapya ya mpira nje ya klabu.