Tyron amepata kazi katika klabu ya Orlando Pirates ya nchini kwao Afrika Kusini na tayari amewasilisha ombi la kutaka kuondoka ili kujiunga na miamba hiyo.
Uongozi wa Simba umefanya jitihada za kumbakisha lakini hitaji lake la kuondoka limekuwa kubwa kutokana maslahi yake lakini pia kuwa karibu na familia yake.
Kwa kipindi cha nusu msimu alichohudumu ndani ya kikosi chetu Tyron ameboresha viwango vya makipa wetu Aishi Manula, Beno Kakolanya na Ally Salim na kuwa gumzo barani Afrika.
Tunamtakia kila la heri kocha Tyron katika majukumu yake mapya, tunatambua thamani yake ambapo mchezo wetu wa mwisho dhidi ya Mbeya Kwanza Jumatano tutautumika kumuaga rasmi.
Katika kuboresha bechi letu la ufundi uongozi umeanza mchakato wa kutafuta mrithi wa Tyron haraka ili kumpata kabla ya kuanza kwa maandalizi ya msimu mpya wa mashindano 2022/23.