Beno alijiunga nasi mwaka 2019 akitokea Yanga akiwa mchezaji huru.
Katika miaka minne aliyodumu na kikosi chetu, Beno amekuwa mchezaji muhimu na mara zote alipopata nafasi ya kucheza alijitoa kwa jasho na damu kuhakikisha timu inapata matokeo chanya.
Advertisement
Uongozi wa klabu unamshukuru Beno kwa utumishi wake uliotukuka kwenye kikosi chetu na tunamtakia heri katika maisha yake mapya ya soka nje ya Simba.
Beno anakuwa mchezaji wa tano kuachana na klabu baada ya Augustine Okrah, Mohamed Ouattara na Victor Akpan.