Simba Sports Club
News

Kuziona Simba, Yanga Jumamosi 'buku' 10

24 May 2022 By simbasc 871 views
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) limetangaza viingilio vya mchezo wa Nusu Fainali ya Michuano ya Azam Sports Federation Cup kati yetu na Yanga ambapo cha chini kitakuwa Sh 10,000. Viingilio hivyo vimetangazwa leo ikiwa ni siku nne kabla ya mchezo wenyewe ili kuwapa nafasi mashabiki kukata tiketi mapema. Mchezo na watani wa jadi huvuta hisia za mashabiki wengi ambapo wengine hutoka nje ya nchi kuja kushuhudia. Hivi hapa viingilio vyenyewe VIP A Sh 30,000 VIP B Sh 20,000 Mzunguko Sh 10,000
Advertisement
Back to homepage
Share this story