Simba Sports Club
News

Kuziona Simba, Al Hilal Buku Mbili

4 Feb 2023 By simbasc 328 views
Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally ametangaza viingilio vya mchezo wetu kirafiki wa kimataifa dhidi ya Al Hilal utakaopigwa kesho Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni ambapo cha chini kitakuwa Sh. 2000. Ahmed amesema viingilio hivyo vinatokana na jana kucheza mechi ya Ligi na watu wamelipa hivyo ili kuwapunguzia majukumu tumeweka kiingilio kidogo ambacho kila mtu atakimudu. Ahmed ameongeza kuwa kesho itakuwa siku ya mtoko wa mwisho wa wiki kwahiyo Wanasimba wanapaswa kuja uwanjani kufurahi na familia ambapo watoto chini ya umri wa miaka 10 wataingia bure. "Jana tumecheza mechi mashabiki walikuja kwa wingi uwanjani. Haitakuwa vizuri kuweka viingilio vikubwa badala yake tunafanya kama mtoko ili Wanasimba waje kwa wingi na familia zao," amesema Ahmed. Viingilio vilivyopangwa VIP A Sh. 10,000 VIP B Sh. 5000 Mzunguko 2000
Advertisement
Back to homepage
Share this story