Zimbwe Jr amesema unapojiandaa na mechi ngumu ya kimataifa inakuwa vizuri kuwa na kikosi kamili ambapo kocha anakuwa na wigo mpana wa kupanga timu.
Wachezaji ambao walikuwa na majeruhi na tayari wamerejea mazoezi ni Kibu Denis, Chris Mugalu, Sadio Kanoute, Jonas Mkude na Aishi Manula.
Advertisement
"Tunaenda kwenye mchezo mgumu, jambo la kushukuru tunaenda tukiwa na kikosi kamili wachezaji wenzetu waliokuwa majeruhi wamerejea na wameongeza nguvu kikosini," amesema Zimbwe Jr.
Zimbwe ameongeza kuwa alama tatu za mchezo wa Jumapili zitaweka wazi mustakabali wetu kwenye kundi na kuongeza morali kuelekea mechi mbili zilizobaki.