Bergman (37) raia wa Afrika Kusini ana leseni B kutoka Shirikisho la Soka barani Ulaya (UEFA) ambayo inamuwezesha kutimiza majukumu yake akiwa katika benchi la ufundi.
Ujio wa Bergman ni chaguo la kocha mkuu Steve Barker ambaye amempendekeza ili kuongeza ufanisi ndani ya benchi la ufundi.
Advertisement
Kabla ya kujiunga nasi Bergman alikuwa akiifundisha timu ya vijana chini ya umri wa miaka 19 ya Mamelodi Sundowns.
Pia amewahi kuwa kocha mkuu katika Kituo cha kukuzia na kuviendeleza vipaji cha Ubuntu Football Academy cha Afrika Kusini.