Inonga aliumia bega katika mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Singida Fountain Gate jijini Tanga, Agosti 10 nakutakiwa kuwa nje kwa wiki mbili.
Kwa upande wake, Kramo aliumia goti mazoezini nakutakiwa kuwa nje ya uwanja kwa muda kidogo ili awe fiti.
Advertisement
Wawili hao pamoja na wenzao wameanza maandalizi ya mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Power Dynamos utakaopigwa Septemba 16, nchini Zambia.