Klabu yetu imeingia mkataba wa miaka miwili na Kocha Pablo Franco (41) raia wa Hispania kukinoa kikosi chetu kuanzia sasa.
Pablo anachukua nafasi ya Didier Gomes raia wa Ufaransa ambaye mkataba wake ulisitishwa wiki mbili zilizopita baada ya makubaliano ya pande zote.
Kabla ya kujiunga nasi Pablo alikuwa anaifundisha Al Qadsia SC ya Quwait kuanzia 2019 hadi 2021.
Mwaka 2015 Pablo alikuwa Kocha Mkuu wa Getafe inayoshiriki Ligi Kuu nchini Hispania.
Pablo ambaye ni muumini wa soka la kushambulia alikuwa Kocha Msaidizi wa Real Madrid mwaka 2018 chini ya Kocha Julen Lopetegui na baadaye Santiago Solari.
Pamoja na kuwa muumini wa soka la kushambulia pia anamudu umiliki wa mpira kwa staili ya Hispania ya pasi nyingi 'tik taka' ambayo ndiyo falsafa ya Simba.
Kocha huyo mwenye Elimu ya UEFA Pro na elimu ya juu ya viungo na usomaji wa michezo, Simba inaamini ujio wake utaongeza ufanisi kwenye eneo lake la ufundi.