Simba Sports Club
News

Kocha wa Makipa amvulia kofia Ally Salim

1 May 2023

Chlouha raia wa Morocco amesema licha ya ujasiri na uwezo mkubwa kitu kingine anachokipenda kutoka kwa Ally ni nidhamu aliyo nayo.

Akizungumzia kiwango alichoonyesha katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Wydad Casablanca, Chlouha amesema Ally amefanya vizuri na hata bao alilofungwa halikuwa kosa lake la moja kwa moja.

Advertisement

"Ni kijana mzuri kwa Simba ya baadaye naona ni mtu sahihi kuchukua nafasi za kaka zake waliopo sasa, amecheza mechi nne kubwa na ameruhusu bao moja pekee.

"Kuhusu bao alilofungwa dhidi ya Wydad juzi, kipa yeyote anaweza kufungwa aina ile ukiangalia Ally hana uzoefu wa kutosha, hajawai kucheza mechi kubwa kama ile ila ameonesha uwezo mkubwa," amesema Kocha Chlouha.

Back to homepage
Share this story