Simba Sports Club
News

Kocha Tyron aenda kuongeza Elimu Afrika Kusini

10 Jun 2022

Kozi hiyo ambayo inahusisha makocha 25 kutoka sehemu mbalimbali duniani ni hatua ya juu zaidi kwenye ukocha ambapo watakuwa na uwezo ya kusoma mchezo pia unawafanya kumshauri kocha mkuu wakati mechi ikiwa inaendelea.

Tyron amesema kozi hiyo itamuwezesha kufundisha majukumu ya magolikipa namna ya kufanya wakiwa na mpira au wasipokuwa nao ili kujua hatari kutoka kwa washambuliaji.

Kocha huyo ameongeza kuwa lengo la kozi hiyo ni kukuza ufundishaji na kuchambua makosa, kutafuta suluhisho na kuwaendeleza magolikipa mmoja mmoja na kwenye timu.

Advertisement

"Nipo kwenye kozi ya juu ya makocha wa magolikipa inayofanyika Afrika Kusini, inahusisha makocha 25 kutoka sehemu mbalimbali duniani lengo ni kuongeza maarifa ya kwenda kuwafundisha makipa.

"Hii ni kozi ya pili inayotolewa na FIFA baada ya ile ya kwanza iliyofanyika mwaka 2016 lengo lake ni kukuza ufundishaji na kuchambua makosa na kuyatafutia ufumbuzi," amesema Tyron.

Back to homepage
Share this story