Simba Sports Club
News

Kocha Gomez afunguka sababu ya kutoa 'dozi kubwa' kwa Mtibwa

14 Apr 2021 By simbasc 1,250 views

Kocha Mkuu, Didier Gomez ameweka wazi sababu ya ushindi wa mabao 5-0 tuliopata dhidi ya Mtibwa Sugar kuwa ni kucheza kwa nidhamu na kujituma.

Licha ya kufahamu Mtibwa haipo kwenye kiwango bora lakini Kocha Gomez aliwataka wachezaji kutowadharau na kucheza kwa nidhamu sababu tulihitaji kupata pointi tatu kwenye mchezo wa leo.

Advertisement

Gomez hakuacha kuwasifia wachezaji kwa kiwango safi walichoonyesha huku akisisitiza kuelekeza nguvu katika mechi tatu za Kanda ya Ziwa.

"Tunafurahi kupata alama tatu ambazo zimezidi kutusogeza kileleni, tulicheza kwa nidhamu na wachezaji walifuata maelekezo tuliyowapa," amesema Kocha Gomez.

Back to homepage
Share this story