Kocha Fadlu amesema ni siku ya kipekee ambayo atalitambulisha benchi lake la ufundi pamoja na kikosi chake atakacho kiongoza kwenye msimu wa mashindano 2024/25.
Fadlu amesema itakuwa ni mara ya kwanza kushiriki Simba Day na atakuwa anakutana na mashabiki moja kwa moja.
"Kiukweli ni jambo kubwa kushiriki Simba Day. Ni siku kubwa na mashabiki wengi wanajitokeza kuja kuiona timu yao."
Advertisement
"Nitapata nafasi ya kulitambulisha benchi langu la ufundi pamoja na kikosi changu, nafikiri itakuwa siku nzuri kwangu," amesema Kocha Fadlu.
Simba Day ya mwaka huu itafanyika Agosti 3 katika Uwanja wa Benjamin Mkapa.