Barker amesema pamoja na malengo hayo lakini tutaiheshimu kila timu tutakayo kutana nayo kwakuwa tunafahamu zimejipanga na zinalitaka taji kama sisi.
Kuhusu maandalizi kocha Barker amesema mazoezi ya siku mbili yaliyofanyika jijini Dar es Salaam na siku mbili za Zanzibar yamempa taswira ya kuendelea kukifahamu kikosi chetu.
"Lazima tuweke malengo kwenye kila mashindano tunayoshiriki, kwa ukubwa tulionao kwetu jambo la kwanza ni kupata ubingwa," amesema Barker.
Wakati huo huo kocha Barker amesema ataitumia michuano ya Kombe la Mapinduzi kuwafahamu wachezaji ili kuweza kujua nini cha kuongeza kwao ili wawe bora zaidi.
Akizungumza kwa niaba ya wachezaji kiungo mkabaji, Hussein Semfuko amewaita mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani kwenye mechi zetu kwa ajili ya sapoti ili kuweza kufanikisha malengo tuliyojiwekea.
"Ili kufanikisha malengo ya kutwaa ubingwa lazima mashabiki watupe sapoti, tunawahitaji na tumejipanga na tupo tayari kuwapa furaha," amesema Semfuko.