Barker amesema maandalizi yote ya mchezo yamekamilika na wachezaji wapo kwenye hali nzuri tayari kwa mchezo huo ambao amekiri utakuwa mgumu.
Barker ameongeza kuwa tumekuwa na ratiba ngumu hasa kutokana na kucheza mechi mfufulizo ugenini lakini hata hivyo tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi ili kuweza kufikia malengo tuliyojiwekea ya kupigania ubingwa.
"Tupo tayari kwa asilimia 100 kuwakabili Pamba Jiji kesho, tunafahamu utakuwa mchezo mgumu hasa kutokana na wapinzani kuwa na matokeo mazuri wakiwa nyumbani lakini tumejiandaa kimwili na kiakili ili kuweza kuwakabili," amesema Kocha Barker.
Kwa upande wake kiungo mshambuliaji, Morice Abraham amesema pamoja na upinzani na ugumu ambao tunatarajia kukutana nao lakini tumejipanga na malengo yetu yanabaki yale yale ya kutafuta alama tatu.
"Tunawaheshimu Pamba na tunategemea watatupa upinzani mkubwa lakini tumejipanga kuwakabili na lengo ni kupata alama tatu," amesema Morice.