Simba Sports Club
News Videos

Kocha Barker afunguka maandalizi mchezo dhidi ya Dodoma

24 Feb 2026

Barker amesema tumejiandaa kukutana na timu ngumu na imara ambayo inacheza vizuri huku tukifahamu wapo nyumbani lakini tumejiandaa kuwakabili.

Barker ameongeza kuwa tunahitaji kuwa na muendelezo wa kupata alama tatu kwenye kila mchezo ili kujiweka katika nafasi nzuri za kupata ubingwa.

"Maandalizi yamekamilika na wachezaji wote wapo kwenye hali nzuri, tunajua tunaenda kukutana na timu ngumu lakini malengo yetu ni kuendelea kupata ushindi," amesema Barker.

Advertisement

Akizungumza kwa niaba ya wachezaji mlinzi wa kulia, David Kameta 'Duchu' amewaomba mashabiki kujitokeza kwa wingi uwanjani kwa ajili ya kuwapa sapoti ili kufikia malengo tuliyojiwekea.

Duchu ameongeza kuwa tunafahamu utakuwa mchezo mgumu kutokana na Dodoma kuwa kwenye kiwango bora lakini tumejipanga kuhakikisha tunapata ushindi ingawa haitakuwa kazi rahisi.

"Sisi kama wachezaji tupo tayari, tunafahamu utakuwa mchezo mgumu na tunatarajia kupata upinzani mkubwa kutoka kwa Dodoma lakini tumejiandaa na tupo tayari," amesema Duchu.

Back to homepage
Share this story