Simba Sports Club
News

Kiungo Mnaigeria atua kufanya majaribio

6 Jan 2022

Kiungo mkabaji, Etop David Udoh raia wa Nigeria ametua nchini kwa ajili ya majaribio na kama atafanya vizuri atakuwa na nafasi ya kusajiliwa moja kwa moja.

Kabla ya kutua nchini, Udoh alikuwa anacheza katika klabu ya Arar FC ya Saudi Arabia inayoshiriki ligi daraja la pili.

Advertisement

Udoh tayari ameungana na kikosi Visiwani Zanzibar na katika mchezo wetu wa jana dhidi ya Selem View alikuwepo jukwaani akifuatilia.

Udoh anakuwa mchezaji wa tatu kuja kufanya majaribio baada ya Sharaf Eldin Shiboub wa Sudan na Moukoro Cheikh Tenena raia wa Ivory Coast ambayo wote wamecheza mechi yetu ya jana.

Back to homepage
Share this story