Simba Sports Club
News

Kikosi Kitakachotuwakilisha dhidi ya Yanga leo

23 Oct 2022 By simbasc 360 views
Mshambuliaji kinara Moses Phiri amepangwa kuongoza mashambulizi katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya watani wetu Yanga utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 11 jioni. Kama kawaida Phiri atapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Clatous Chama, Pape Sakho na Augustine Okrah. Mchezaji mwandamizi Jonas Mkude ataongoza safu ya kiungo wa ulinzi ambapo atacheza sambamba na Mzamiru Yassin. Kikosi kamili kilivyopangwa Aishi Manula (28), Israel Patrick (5), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Pape Sakho (10), Mzamiru Yassin (19), Moses Phiri (25), Clatous Chama (17), Augustine Okrah (27). Wachezaji wa akiba Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Nassor Kapama (35), Peter Banda (11), John Bocco (22), Habibu Kyombo (32), Kibu Denis (38).
Advertisement
Back to homepage
Share this story