Simba Sports Club
News

Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya Yanga leo

13 Aug 2022 By simbasc 555 views
Kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa moja usiku kuikabili Yanga kwenye mchezo wa Ngao ya Jamii kuashiria kufunguliwa kwa pazia la Ligi Kuu ya NBC Msimu wa 2022/23. Habib Kyombo ataongoza mashambulizi akisaidiwa na Clatous Chama, Pape Sakho na Kibu Denis. Jonas Mkude na Sadio Kanoute watasimama katika kiungo wa ulinzi huku Henock Inonga na Mohamed Ouattara wakiongoza idara ya ulinzi. Kikosi Kamili kilivyopangwa Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5), Mohamed Hussein (5), Henock Inonga (29), Mohamed Ouattara (33), Jonas Mkude (20), Pape Sakho (10), Sadio Kanoute (13), Habib Kyombo (32), Clatous Chama (17), Kibu Denis (38). Wachezaji wa akiba Ally Salim (1), Shomari Kapombe (12), Joash Onyango (16), Victor Akpan (6), Augustine Okrah (28), Mzamiru Yassin (19), Dejan (7), John Bocco (22) Nelson Okwa (8).
Advertisement
Back to homepage
Share this story