Simba Sports Club
News

Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya Mbeya City leo

23 Nov 2022 By simbasc 388 views
Nahodha John Bocco ataendelea kuongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa leo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Uwanja wa Sokoine saa 10 jioni. Katika mchezo uliopita ambao tuliibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Ruvu Shooting Bocco aliongoza mashambulizi na kupiga hat trick. Bocco atasaidiana na kinara Moses Phiri ambapo wapata msaada kutoka kwa viungo wawili washambuliaji Clatous Chama na Augustine Okrah. Kikosi kamili kilivyopangwa Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), John Bocco (22), Moses Phiri (25), Augustine Okrah (27). Wachezaji wa Akiba Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Mohamed Ouattara (33), Victor Akpan (6), Pape Sakho (10), Habibu Kyombo (32), Kibu Denis (38).
Advertisement
Back to homepage
Share this story