Simba Sports Club
News

Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya KVZ leo

5 Jan 2023 By simba 434 views
  Kocha Juma Mgunda amefanya mabadiliko ya mchezaji mmoja katika kikosi kitakachoanza leo dhidi ya KVZ kulinganisha na kile kilichoanza na Mlandege. Mgunda amemuanzisha kiungo Victor Akpan ambaye mchezo uliopita alitokea benchi huku kiungo mshambuliaji Kibu Denis aliyeanza akipumzishwa. Mshambuliaji Habib Kyombo ataendelea kuongoza mashambulizi huku akisaidiwa na Nelson Okwa, Michael Joseph na Augustine Okrah. Kikosi Kamili kilivyopangwa Beno Kakolanya (30), Jimmyson Mwanuke (21), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Nassor Kapama (35), Jonas Mkude (20), Victor Akpan (6), Nelson Okwa (8), Habibu Kyombo (32), Michael Joseph (45) Augustine Okrah (27) Wachezaji wa Akiba Ally Salim (1), Maulid Juma (50), Pasco Yasita (54), Omary Mfaume (53), Hassan Mussa (52), Joseph Mbaga (49), Seif Suleiman (36).
Advertisement
Back to homepage
Share this story