Simba Sports Club
News

Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya KMC Leo

26 Dec 2022 By simba 266 views
  Nahodha John Bocco ataendelea kuongoza safu ya ushambuliaji katika mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya KMC utakaopigiwa leo saa 10 jioni Uwanja wa CCM Kirumba. Baada ya kukosekana kwa kinara Moses Phiri leo kocha Juma Mgunda amewapanga viungo watatu washambuliaji kumsaidia Bocco. Sadio Kanoute na Mzamiru Yassin kama kawaida wataendelea kuongoza safu ya kiungo wa walinzi huku Joash Onyango na Henock Inonga wakisimama kama walinzi wa kati. Kikosi Kamili kilivyopangwa Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Sadio Kanoute (13), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), John Bocco (22), Pape Sakho (10), Augustine Okrah (27). Wachezaji wa Akiba Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Mohamed Ouattara (33), Victor Akpan (6), Nelson Okwa (8), Habibu Kyombo (32), Kibu (38).
Advertisement
Back to homepage
Share this story