Simba Sports Club
News

Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya Horoya Leo

18 Mar 2023 By simbasc 367 views
Kikosi chetu leo saa moja usiku kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili Horoya kutoka Guinea katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi. Kocha Mkuu, Roberto Oliviera 'Robertinho' amefanya mabadiliko ya mchezaji mmoja ukilinganisha na kikosi kilichocheza mchezo wa mwisho dhidi ya Mtibwa Sugar. Robertinho amemuanzisha Kibu Denis akichukua nafasi ya Moses Phiri ambaye atatokea benchi. Kikosi kamili kilivyopangwa Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12),  Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Sadio Kanoute (13), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), Jean Baleke (4), Saido Ntibazonkiza (39), Kibu Denis (38). Wachezaji wa Akiba Beno Kakolanya (30), Israel Patrick (5),  Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Peter Banda (11), Habibu Kyombo (32), John Bocco (22), Moses Phiri (25), Pape Sakho (10).
Advertisement
Back to homepage
Share this story