Simba Sports Club
News

Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya Geita Leo

18 Dec 2022 By simba 327 views
  Kocha Juma Mgunda, amewapanga nahodha, John Bocco na Moses Phiri kuongoza mashambulizi katika mchezo wa leo wa Ligi Kuu ya NBC dhidi Geita Gold utakaopigwa Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza saa 10 jioni. Bocco na Phiri wametengeneza muelewano mzuri na imekuwa chachu ya ushindi tunaendelea kupata katika mechi zetu. Wawili hao watapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji, Clatous Chama na Pape Sakho ambao watashambulia kutokea pembeni. Kikosi kamili kilivyopangwa Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Sadio Kanoute (13), Clatous Chama (17), Mzamiru Yassin (19), Bocco (22), Moses Phiri (25), Pape Sakho (10). Wachezaji wa Akiba Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Kennedy Juma (26), Mohamed Ouattara (33), Jonas Mkude (20), Victor Akpan (6), Kibu Denis (38), Habibu Kyombo (32), Augustine Okrah (27).
Advertisement
Back to homepage
Share this story