Simba Sports Club
News

Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya De Agosto leo

9 Oct 2022

Katika mtanange dhidi ya Dodoma Jiji, Inonga alipata maumivu wakati wa kupasha misuli kabla ya kuanza mchezo hali iliyosababisha kuwekwa pembeni lakini sasa yuko kamili na ataongoza idara ya ulinzi akiwa na Joash Onyango.

Moses Phiri ataendelea kuongoza idara ya ushambuliaji ambapo atapata msaada wa karibu kutoka kwa Augustine Okrah, Clatous Chama na Kibu Denis.

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Advertisement

Aishi Manula (28), Israel Patrick (5), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Sadio Kanoute (13), Augustine Okrah (27), Mzamiru Yassin (19), Moses Phiri (25), Clatous Chama (17), Kibu Denis (38).

Wachezaji wa Akiba

Beno Kakolanya (30), Erasto Nyoni (18), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Jonas Mkude (20), Pape Sakho (10), Nassor Kapama (35), John Bocco (22), Habibu Kyombo (32).

Back to homepage
Share this story