Simba Sports Club
News

Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya CSKA Moscow Leo

15 Jan 2023 By simba 359 views
  Nahodha John Bocco, ataendelea kuongoza mashambulizi katika mchezo wetu wa mwisho wa kirafiki hapa Mjini Dubai dhidi ya CSKA Moscow ya Urusi utakaopigwa Abu Dhabi saa tisa Alasiri. Kama ilivyokuwa katika mchezo uliopita dhidi ya Al Dhafrah, Bocco atapata msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Clatous Chama, Saido Ntibazonkiza na Pape Sakho. Katika eneo la kiungo wa ulinzi kocha Mkuu Roberto Oliviera 'Robertinho' amempanga Erasto Nyoni pamoja na Sadio Kanoute. Kikosi kamili kilivyopangwa Aishi Manula (28), Shomari Kapombe (12), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Mohamed Ouattara (33), Erasto Nyoni (18), Pape Sakho (10), Sadio Kanoute (13), John Bocco (22), Saido Ntibazonkiza (39), Clatous Chama (17). Wachezaji wa Akiba Beno Kakolanya (30), Ally Salim (1), Jimmyson Mwanuke (21), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Nassor Kapama (35), Jonas Mkude (20), Mzamiru Yassin (19), Habibu Kyombo (32), Kibu Denis (38)
Advertisement
Back to homepage
Share this story