Simba Sports Club
News

Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya Coastal Leo

9 Jun 2023 By simbasc 149 views
Leo 9:30 Alasiri kikosi chetu kitashuka katika Uwanja wa Uhuru kuikabili Coastal Union katika mchezo wa Ligi ya NBC ambao utakuwa wa mwisho katika msimu wa 2022/23. Kocha Roberto Oliviera 'Robertinho' amefanya mabadiliko ya mchezaji wawili ukilinganisha na kikosi kilichocheza juzi dhidi ya Polisi Tanzania. Robertinho amewaanzisha Nassor Kapama na John Bocco wakichukua nafasi za Henock Inonga na Jean Baleke. Kikosi Kamili kilivyopangwa: Ally Salim (1), Shomari Kapombe (12), Israel Patrick (5), Kennedy Juma (26), Erasto Nyoni (18), Nassor Kapama (35), Peter Banda (11), Jonas Mkude (20), John Bocco (22), Saido Ntibanzonkiza (39), Kibu Denis (38). Wachezaji wa Akiba Beno Kakolanya (30), Ahmed Teru (31), Gadiel Michael (2), Mohamed Mussa (14), Jean Baleke (4), Habib Kyombo (32), Jimmyson Mwanuke (21)
Advertisement
Back to homepage
Share this story