Simba Sports Club
News

Kikosi kitakachotuwakilisha dhidi ya Azam leo

27 Oct 2022

Katika mechi kadhaa zilizopita Mgunda amekuwa akimtumia Phiri kwenye safu ya ushambuliaji huku akiwa na viungo watatu washambuliaji.

Kwenye mchezo wa leo Kyombo na Phiri watapewa msaada wa karibu kutoka kwa viungo wawili washambuliaji Clatous Chama na Augustine Okrah ambao watatokea pembeni.

Kiraka Erasto Nyoni amepangwa kucheza beki wa kulia akichukua nafasi ya Israel Patrick aliyepata majeraha wakati Shomari Kapombe hali yake ikiendelea kuimarika.

Katika idara ya kiungo wa ulinzi Jonas Mkude amepangwa pamoja na Nassor Kapama.

Advertisement

Kikosi kamili kilivyopangwa

Aishi Manula (28), Erasto Nyoni (18), Mohamed Hussein (15), Joash Onyango (16), Henock Inonga (29), Jonas Mkude (20), Clatous Chama (17), Nassor Kapama (35), Habibu Kyombo (32), Moses Phiri (25), Augustine Okrah (27).

Wachezaji wa Akiba

Beno Kakolanya (30), Gadiel Michael (2), Kennedy Juma (26), Mohamed Ouattara (33), Victor Akpan (6), Peter Banda (11), John Bocco (22), Kibu Denis (38), Pape Sakho (10).

Back to homepage
Share this story