Simba Sports Club
News

Kikosi kitakacho tuwakilisha dhidi ya Asante Kotoko Leo

28 Aug 2022 By simba 608 views

Moses Phiri ataendelea kuongoza idara ya ushambuliaji katika mchezo wetu wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Asante Kotoko kutoka Ghana utakaopigwa Uwanja wa Al Hilal nchini Sudan.

Phiri atapa msaada wa karibu kutoka kwa viungo washambuliaji Clatous Chama, Pape Sakho na Agustine Okrah.

Nassor Kapama na Victor Akpan watasimama katika kiungo wa ulinzi wakati mabeki wakati ni wale wale Henock Inonga na Mohamed Ouattara.

Advertisement

Kikosi Kamili kilivyopangwa

Ally Salim (1), Israel Patrick (5), Gadiel Michael (2), Henock Inonga (29), Mohamed Ouattara (33), Nassor Kapama (35), Pape Sakho (10), Victor Akpan (6), Moses Phiri (25), Clatous Chama (17), Augustine Okrah (27).

Wachezaji wa Akiba

Ahmed Feruzi (31), Jimmyson Mwanuke (21), Nelson Okwa (8), Dejan Georgijevic (7), Peter Banda (11)

Back to homepage
Share this story