Kikosi kilianza mazoezi tangu Juni 6 kwa wachezaji ambao hawakuwa katika majukumu ya timu za taifa lakini leo kimekamilika na wote wamejumuika.
Maandalizi ya mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Mbeya City utakaopigwa Juni 16 yanaendelea vizuri na kila kitu kipo sawa.
Advertisement
Morali ya wachezaji ipo juu na kila mmoja amejitahidi kuonyesha jitihada mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kumuamini.