Kwa siku tatu mfululizo kikosi chetu kimeendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo ujao wa Klabu Bingwa Afrika dhidi ya AS Vita utakaopigwa Uwanja wa Benjamin Mkapa Aprili 3, mwaka huu.
Mazoezi yanafanyika chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomez huku wachezaji kutoka timu ya wakubwa wakiwa tisa pekee wengine wakiwa chini ya umri wa miaka 20.

Kwa mara ya kwanza tumetoa wachezaji 18 kwenda kwenye timu zao za taifa tukiwa tumeandika historia kwani haijawahi kutokea kabla kitu ambacho kimemfanya Kocha Gomez kuhitaji kufanya mazoezi pamoja na timu ya vijana.
Mara tu wachezaji 18 waliopo kwenye majukumu ya timu zao taifa kumaliza watarejea mara moja kujiunga na wenzao na maandalizi ya pamoja yatafanyika kuivaa Vita.
Tutaingia kwenye mchezo huo tukiwa vinara wa kundi A kwa pointi ambapo tunahitaji ppinti moja pekee kujihakikishia kuingia Robo Fainali ya Michuano ya Klabu Bingwa tukisaliwa na mechi mbili.