Simba Sports Club
News

Kikosi chawasili salama Zanzibar

19 Mar 2024

Tumesafiri na wachezaji wote ambao hawako kwenye majukumu ya timu za Taifa lengo likiwa kuwaweka tayari na mchezo huo mkubwa ambao tunahitaji kupata ushindi.

Baada ya kikosi kufika Zanzibar leo saa tatu usiku kitafanya mazoezi ya utimamu wa mwili kwa ajili ya kuweka miili sawa na kesho kitaendelea na programu ya mazoezi.

Advertisement

Tumechagua kuweka kambi Zanzibar kutokana na utilivu wake huku pia kukiwa na nafasi ya timu kufanya mazoezi usiku.

Back to homepage
Share this story