Simba Sports Club
News

Kikosi chawasili salama Niger

19 Feb 2022

Simba imewasili Niamey saa nane mchana kwa saa za Niger ambayo ni sawa na saa 10 jioni kwa saa za Afrika Mashariki na Kati.

Baada ya kuwasili Niger moja kwa moja kikosi kimekwenda hotelini kwa ajili ya mapumziko mafupi ya wachezaji.

Advertisement

Baada ya mapumziko mafupi kikosi kitafanya mazoezi saa 11 jioni kwa saa za Niger na saa moja usiku kwa saa za nyumbani katika Uwanja wa General Seyni Kounteche ambao utatumika kwenye mchezo huo.

Mchezo dhidi ya Us Gendermarie utachezwa saa 11 Jioni kwa saa Niger sawa na saa moja usiku kwa saa za Afrika Mashariki ambapo utachezeshwa na Waamuzi kutoka Eritrea na Ethiopia.

Back to homepage
Share this story