Kikosi chetu kimefanya mazoezi ya mwisho katika Uwanja wa Mao Tse Tung kujiandaa na mchezo wa kwanza wa Michuano ya Mapinduzi dhidi ya Selem View utakaopigwa Uwanja wa Amani kesho Jumatano saa 10:15 jioni.
Wachezaji wote waliopo kikosini wamefanya mazoezi na wako tayari kwa mchezo huo ambao tunaamini utakuwa mgumu.
Advertisement
Kila mchezaji amejitahidi kuonyesha uwezo mkubwa mazoezini ili kulishawishi benchi la ufundi kumpa nafasi.
Bila kuangalia jina au ukubwa wa wapinzani, tutaingia uwanjani kwa tahadhari na kuwaheshimu wapinzani sababu lengo letu ni kushinda.