Simba Sports Club
News

Kikosi chaendelea kujifua nchini Zambia

6 Dec 2021

Kikosi chetu kimefanya mazoezi jioni katika uwanja wa Zanaco kujiweka sawa ili tukirejea nyumbani tuwe katika ubora ule ule tuliokuwa nao awali.

Jana tulifanikiwa kutinga hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Afrika kwa jumla ya mabao 4-2 baada ya mechi zote mbili tukishinda 3-0 nyumbani na kupoteza 2-1 ugenini.

Advertisement

Asubuhi kikosi kilifanya mazoezi Gym kwa ajili ya kuweka miili sawa baada ya mechi ya jana ya marudiano ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Red Arrows.

Timu inatumia mazoezi haya kama sehemu ya maandalizi ya mchezo wetu wa Ligi Kuu ya NBC unaofuata ambao tutacheza Jumamosi dhidi ya watani wetu Yanga.

Back to homepage
Share this story