Baada ya mapumziko ya wiki moja kikosi kimerejea mazoezini jioni ya leo kwenye viwanja vyetu vya Mo Simba Arena kwa ajili ya kujiweka fiti kujiandaa na mechi zilizo mbele yetu.
Wachezaji walioanza mazoezi ni tisa wakiwa pamoja na kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 20 kutokana na nyota wengi kuitwa kwenye timu zao za Taifa.
Advertisement

Safari hii tumeweka rekodi ya kutoa wachezaji 18 walioitwa kwenye timu zao Taifa kwa pamoja ikiwa haijawahi kutokea kabla.