Kikosi chetu cha Timu ya Wanawake Simba Queens kitashuka katika Uwanja wa Benjamin Mkapa saa 10 jioni kuikabili Yanga Princess kwenye mchezo wa Serengeti Lite Women's Premier league.
Nyota wetu wapya tuliowasajili Pambani Kuzoya na Olaiya Barakat wamepangwa kuanza pamoja na Oppah Clement na Asha Djafar katika idara ya ushambuliaji.