Simba Sports Club
News

Kibu: Ushangiliaji wa Raja ulinipa 'mzuka'

2 Apr 2023

Akizungumza na Simba App, Kibu amesema kelele na nyimbo za mashabiki wa Raja ambao walikuwa wanashangilia muda wote zilikuwa zinampa morali ya kucheza vizuri.

Kibu ameongeza kuwa anatamani mashabiki wetu wafikie viwango vya ushangiliaji kama Raja kwakuwa inaongeza hamasa na kuwapa nguvu wachezaji uwanjani.

“Hata sisi tuliposawazisha bao mashabiki wao hawakuacha kuimba na wala hawakuwa wanyonge waliendelea kushangilia mwanzo mwisho, hili ni jambo zuri."

Advertisement

"Kuna wakati mpira ukisimama nilikuwa nawaangalia namna wanavyofanya kiukweli inavutia sana halafu hawashangilii matukio kama vile tobo au kanzu wenyewe wanaimba kwa mtiririko wao ule ule," amesema Kibu.

Kibu ametoa ushauri kwa kitengo cha Habari kutengeneza kundi la mashabiki wenye uwezo wa kushangilia muda wote wa mchezo bila kujali matokeo akisema hali hiyo itaongeza morali kwa wachezaji.

Back to homepage
Share this story