Simba Sports Club
News

Kibu nje wiki moja

28 Feb 2023

Daktari wa timu, Edwin Kagabo amesema Kibu amepata maumivu ya mguu na baada ya vipimo anahitajika kuwa nje kwa muda wa wiki moja ili kupona kabisa.

"Kibu amepata maumivu katika mchezo uliopita dhidi ya Vipers, haikuwa mbaya sana lakini inabidi akae nje ya uwanja kwa wiki moja kabla ya kuanza mazoezi," amesema Dk. Edwin.

Advertisement

Wakati huo huo kiungo mshambuliaji, Augustine Okrah ameanza mazoezi mepesi chini ya uangalizi kabla ya kujiunga pamoja na wenzake.

Back to homepage
Share this story