Simba Sports Club
News

Kibu mchezaji bora Mei

2 Jun 2022 By simbasc 932 views
Kiungo mshambuliaji, Kibu Denis amechaguliwa mchezaji bora wa mashabiki wa mwezi Mei (Emirate Aluminium ACP Simba Fans Player of the Month). Kibu ameshinda tuzo hiyo baada ya kuwapiku viungo Rally Bwalya pamoja na Mzamiru Yassin. Katika mwezi Mei, Kibu amecheza mechi saba sawa na dakika 630 akifunga mabao matano na kusaidia kupatikana kwa bao moja. Kwa kushinda kinyang'anyiro hicho Kibu atakabidhiwa pesa taslimu Sh. 2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP. Mchanganuo wa kura Jina Kura Asilimia Kibu 474 84 Bwalya 67 11 Mzamiru 19 3
Advertisement
Back to homepage
Share this story