Wachezaji hao ni viungo washambuliaji Kibu Denis na Rally Bwalya pamoja na kiungo mkabaji Mzamiru Yassin.
Walinzi wa kati Henock Inonga na Joash Onyango waliingia tano bora lakini baada ya kuchujwa wamebaki nyota hao watatu waliotinga fainali.
Mchanganuo wa takwimu zao za mwezi Mei.
Mechi dakika Goli Assist
1. Kibu 7 630 5 1
Advertisement
2. Bwalya 7 508 1 4
3. Mzamiru 6 465 0 0
Zoezi la kupiga kura kwa mashabiki tayari limeanza kupitia tovuti yetu ya www.simbasc.co.tz na litakamilika Juni Mosi saa sita usiku.
Mshindi wa jumla atakabidhiwa kitita cha Sh.2,000,000 na tuzo kutoka kwa wadhamini Emirate Aluminium ACP.