Kibu alikuwa amebakisha miezi sita katika mkataba wake na klabu ambapo sasa anakwenda kupata changamoto mpya nchini Libya.
Kibu alijiunga nasi mwaka 2021akitokea Mbeya City ambapo katika kipindi chote cha miaka minne na nusu amekuwa mchezaji muhimu wa kikosi cha kwanza.
Kibu atakumbukwa kwa jinsi alivyokuwa anajituma muda wote uwanjani kwa ajili ya kuisadia timu kupata matokeo na mara zote amekuwa mpambanaji halisi.
Advertisement
Kibu ameyatumia mazoezi ya leo kuagana na wachezaji pamoja na benchi la ufundi.
Uongozi wa klabu unamtakia kheri Kibu katika maisha yake mapya nje ya Simba na una matumaini kuwa nyota huyo wa Taifa Stars atakuwa na mchango mkubwa katika timu hiyo.