Simba Sports Club
News

Kibegi kupigwa Mnada leo Usiku

31 Jul 2023

Jezi hizo zina majina ya Viongozi wetu wakuu wa nchi mgongoni ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Hussein Mwinyi, Makamu wa Rais, Dk. Phillip Mpango.

Nyingine zimeandikwa majina ya Makamu wa Rais, Majaliwa Kassim Majaliwa, Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Tulia Akson pamoja na Rais wa Heshima wa Klabu, Mohamed Dewji 'Mo'.

Advertisement

Pesa ambazo zitapatikana kwenye mnada wa leo zitatumika katika ujenzi wa wodi za mama na mtoto kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali ya Zanzibar.

Uongozi wa Klabu unawakaribisha Wanasimba wote kushiriki mnada wa leo ili kupatikana kwa pesa ambazo zitatumika kwa malengo tajwa.

Back to homepage
Share this story