Simba Sports Club
News

Kibegi chashuka Mlimani chapokelewa na Waziri Nape

22 Jul 2023

Waziri Nape alikuwa pamoja na Meneja Habari na Mawasiliano wa klabu, Ahmed Ally wakati wa kuwapokea mashujaa hao wakiwa na Kibegi.

Wakati wanaanza safari ya kupanda Mlima walikabidhiwa bendera na Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Mh. Abdallah Mwaipaya na leo wameshuka wamepokelewa na Waziri Nape.

Advertisement

Kama ilivyotangazwa awali jezi za mfano ambazo zimeandikwa majina ya Viongozi wa Serikali na kupekekwa hadi kilele cha Mlima Kilimanjaro zitapigwa mnada.

Pesa zitakazopatikana kwenye mnada huo zitajenga Wodi ya wazazi katika Hospitali ya Taifa Muhimbili pamoja na Hospitali ya Taifa Zanzibar.

Back to homepage
Share this story