Simba Sports Club
News

Kennedy, Israel wajiunga na timu Zanzibar

2 Jan 2024

Wawili hao walikuwa katika kikosi cha awali cha Stars kilichoitwa kwa ajili ya michuano ya AFCON lakini baada ya mchujo hawakujumuishwa hivyo wamejiunga na timu.

Kennedy na Israel wameshiriki katika mazoezi ya mwisho ya kujiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya Singida Fountain Gate yaliyofanyika Uwanja wa nje wa New Amaan Complex.

Advertisement

Kennedy na Israel wanakifanya kikosi chetu kiwe na wachezaji 22 ambao tutawatumia kwa ajili ya michuano hii ya Mapinduzi.

Back to homepage
Share this story