Mlinzi wa kati Kennedy Juma, anesema anajisikia furaha kucheza katika Uwanja wa CCM Kirumba kwa sababu historia yake ya soka ndipo ilipoanzia.
Kennedy ni mmoja wa wachezaji wetu 24 waliopo hapa jijini Mwanza tayari kwa mchezo wa kesho wa Ligi Kuu ya NBC dhidi ya Ruvu Shooting.
Kannedy ambaye ni mwenyeji wa Sengerema amesema anakuwa nafuraha kila anapocheza katika uwanja huo kwa kuwa familia yake huwa inahudhuria kumpa sapoti.
"Mimi Mwanza ni nyumbani, tunapoishi si mbali na hapa uwanjani kwa hiyo kila nikifika huku najisikia furaha sana. Hata familia yangu huwa inakuja kwa ajili ya kunipa sapoti," amesema Kennedy.
Kennedy amewaomba mashabiki wetu kujitokeza kwa wingi kesho kwa ajili ya kuisapoti timu lengo likiwa kuhakikisha tunaondoka na alama zote tatu.
"Tunajua Simba tuna mashabiki wengi hivyo tunawaomba kujitokeza kwa wingi kesho, sisi kama wachezaji tumejipanga na tupo tayari kuwapa furaha," amesema Kennedy.